Kwa wale waliokuwa wanazichukia vuvuzela za Afrika Kusini itabidi wabadili mtazamo wao... Kwani inaelekea zinaweza kutumika kama alama ya upenzi wa mpira wa miguu au timu ya mpira wa miguu.
Ujerumani ambayo ilikuwa maarufu kupitia pweza wake waliyempachika jina la Paul, inaendelea kuwa maarufu zaidi bada ya kampuni moja huko kutaka kutengenezewa vuvuzela kwa makadirio ya awali waweke oda ya vuvuzela milioni 5 (5,000,000). Kwa sasa bado wapo kwenye mchakato mkubwa wa kuweza kubuni vuvuzela ambayo itakubalika kwenye soko lao.
Inapenda kufanya mabadiliko kidogo kutokana na vuvuzela za Afrika kusini, kwani inadaiwa zile za Sauzi, zimetengenezwa kwa plastic hafifu (cheap plastic), na wao hawawezi kuzipata hizo. Pia za kwao wanataka ziwe na uwezo wa kutokuharibu mazingira (environmental friendly).
Pia inapenda vuvuzela zao ziwe na rangi 3 kama ilivo bendera ya nchi yao, yaani nyeusi, manjano na nyekundu, na pia iwe nyepesi zaidi ambayo itapunguza gharama za usafiri.
Kwa kuzingatia malalamiko ya wanachi wa Ujerumani, ya kuwa walipokuwa wanaangalia runinga wakati wa kombe la dunia, vuvuzela zilikuwa zinavuma kama vile jamii fulani ya nyuki... kampuni hiyo inataka kubuni vuvuzela ambayo itakuwa na kipunguza sauti (Silencer) ili isiwe kero kwa mashabiki watakaokuwa karibu na hiyo vuvuzela.
Wataalamu wa vuvuzela wa Sauzi wamekuwa wakisisitiza kuwa vuvuzela nzuri ni ile kubwa, lakini wajua ukubwa wa vuvuzela, maana yake sauti yake nayo inakuwa kubwa, nafikiri ndio maana hao jamaa wanataka kipunguza sauti....
Namkumbuka rafiki yangu
Fadhy amabye ana matumaini makubwa sana kwamba vuvuzela zitakuja kuwa maarufu sana, hasa kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.