![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_hBOOJBOudUxGaWUJlP173Qhk7AjLTUSNXavf0kYYzD6nQRVtFFyvtK1BtVLAwE6NZ4uTZPaGSgIKDO5FVQSbhPogw65pFZbxVuISfOsT6e7ofBn0Z-qlypYPQMWxmgUmec6QlvDpbhk/s280/volcano+clouds.jpg)
Kufuka kwa moshi na vumbivumbi la volkeno iliyolipuka huko Iceland kumesababisha hasara kubwa kwa mashirika ya ndege huko Ulaya kaskazini magharibi baada ya kufuta safari nyingi za kuruka na kutua kwenye viwanja vilivyoko huko baada ya moshi mzito wa volkano hiyo kutanda angani.
Hali hii imesababisha hofu kwa mashirika ya ndege kupita karibu na moshi huo ambao unahofiwa unaweza kuingia kwenye injini za ndege aina ya jet na kuweza kusababisha mlipuko au kuzimika ghafla kwa injini hizo na hivyo kusababisha kuanguka kwa ndege.
Wataalamu wa masuala ya jeolojia na afya wameshauri watu wakae ndani pale vumbi hilo litakapoanza kuanguka chini maana linaweza kuwa na madhara kiafya.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhEWDlYTZUiP6wUgsjtBOhiXD7bwBU1VYM9LTsIoRhvixz3Eki5-IfEF5gBHWnTbl7JP3izdFNfHBfgY2rm3s1jofa5SBzxKlX9JGLJlZtw7cclAAabDfS5t1zJW2VITRgdKBu9bGV4eQw/s280/stranded+passengers.jpg)
Habari kutoka msnbc
hi chib! i was just thinking about you a few days ago. i see you have been traveling! i hope all is well with you! welcome back to blogland! joyce
ReplyDeletePoleni ndugu zetu. Naona Africa imesalimika kwa majanga haya ya asili
ReplyDeletewewe uoni mafuriko na vimbunga????
ReplyDeletenaomba kuuliza kama volcano ina uhusiano wowote na gulobally woming a.k.a climate change. kuuliza si upumbavu, bali harakati za kuondoa ujinga na upuuzi kichwani
@ Kamala, mie sina ujuzi sana na mambo ya jeolojia, kwa kutokujua kwangu, nafikiri labda hakuna au upo kidogo sana. Waatalamu wanaweza kutusaidia
ReplyDeletetuombeane ndicho kilichobaki!
ReplyDelete