![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhdXh6Kd-tIxiAlhVgIM7M_GKFFWk7tvWqDEJHUXCqLpCqTxGQwldp-0B2y73fNULDvK-F_jvCWKsjfljkeJz-pVEQH6YSFGe1zCBcT6EeglNeASUbDMI5sd8Xy2VZmXMEWcT9yqD6ZpwU/s280/Darasa.jpg)
And sitting very close to the writing board is unhealthy!!
Baada ya hapo tunategemea watoto wetu waweze kufanya vizuri kama wale ambao wana kila kitu cha kuwasaidia kupata elimu. Kinachonitisha zaidi ni jinsi walivyokaa karibu kabisa na ubao, maana yake wakitumia chaki kuandika halafu mtu afute... vumbi lote linaingia ndani ya macho na pua, baada ya hapo wanapotea darasani wakiwa wagonjwa.
Kazi tunayo!:-(
ReplyDeletePamoja na kukosa sehemu nzuri ya kukaa lakini watoto wanaenda tu shule. Ila sidhani kama hapo kinaingia kitu kichwani. Inasikitisha sana na sijui serikali inafanya nini? Ufisadi tu, kuchukua pesa na kuwapeleka watoto wao kwenye shule nzuri.Naacha isije nikasema nisichotaka kusema.
ReplyDeleteHii ni balaa ya baradhuli. Poor pupils!!
ReplyDeletePamoja na kusoma katika mazingira magumu namna hii, pamoja na kufundishwa katika lugha ambayo siyo yao na pengine wasiyoifahamu vizuri, pamoja na kuwa na kazi nyingi nyumbani kiasi kwamba hawana muda wa kujisomea, pamoja na kufundishwa na walimu ambao wenyewe pengine hawana uhakika sana na wakifundishacho kwa sababu nao hawakufanya vizuri katika mitihani yao (ndiyo maana wakaishia kuwa walimu), pamoja na ukweli kwamba pengine baadhi yao hapo walipo wana njaa, pamoja na kwamba pengine wengine ni mayatima na hawana familia zenye upendo, pamoja na...watoto hawa bado wanakwenda shuleni kwa sababu wanaamini kwamba elimu pekee ndiyo itakayowakomboa. Na kweli utakuta baadhi ya watoto hawa wanasoma mpaka kufika chuo kikuu. Je, ingekuwaje kama wangekuwa na kila kitu kama wenzao katika sehemu nyingine duniani?
ReplyDeleteNa pengine swali la msingi ni hili: ni kweli nchi yao ni masikini kiasi kwamba haiwezi kuwanunulia angalau vidawati vya kukalia? Au wajanja wachache weshatumia pesa za kununulia vidawati kujijengea mahekalu au kwenda vekesheni Ulaya na familia zao? Kuna anayewaonea uchungu? Nani awapiganie?
Nanukuu swali la Profesa kuwa "ni kweli nchi yao ni masikini kiasi kwamba haiwezi kuwanunulia angalau vidawati vya kukalia?"
ReplyDeleteJibu ni kuwa WATAWALA WAO NDIO MASKINI WA FIKRA NA AKILI ZAO WASIOJUA KUWA WANACHOPUUZA KUWEKEZA NDICHO CHA MUHIMU KULIKO MARADHI WANAYOJITAFUTIA KWA KUJILIMBIKIZIA MALI NA KULA VISIVYOHITAJIKA MIILINI MWAO.
Kiama chao chaja.
Beautiful picture! It's exciting to see the kids studying, defying the odds to build a better future.
ReplyDeleteMy best regards from Buenos Aires
Pablo Aro Geraldes, an Argentine friend...
Nakubaliana na wote, nchi zetu zimekuwa maskini kwa umaskini wa fikra za hao wanaoitwa viongozi.
ReplyDeletePablo, you are welcome!
調子が悪いです。 [url=http://ci2s.org/viagura.htm]バイアグラ[/url] バイアグラ 個人輸入
ReplyDeleteIch tue Abbitte, es kommt mir ganz nicht heran. levitra viagra generika [url=http//t7-isis.org]viagra ohne rezept[/url]
ReplyDeleteme parece esto la frase magnГfica http://nuevascarreras.com/cialis/ comprar cialis en mexico Come curiosi .. :) [url=http://nuevascarreras.com/tag/cialis-online/ ]comprar cialis generico [/url]
ReplyDeleteClaro sois derechos. En esto algo es y es el pensamiento excelente. Es listo a apoyarle. http://nuevascarreras.com/tag/cialis/ cialis E vi ГЁ un altro modo? [url=http://nuevascarreras.com/ ]cialis generico comprar [/url]
ReplyDeletePienso que no sois derecho. Soy seguro. Lo discutiremos. [url=http://csalamanca.com/tag/comprar-viagra/ ]viagra 100 mg pfizer [/url] Todo sobre uno y tan infinitamente http://csalamanca.com/tag/comprar-viagra/ viagra generico comprar
ReplyDelete