Siasaaaa
Siasa kwa kweli ni mchezo wa kujaribu kuvutia na kufanikiwa kuteka fikra za wafuasi na watu wengine.
Pia siasa unaweza kuitafsiri kama ni dhana au mawazo aliyonayo mtu, na kujaribu kuwa aminisha watu wengine, ya kuwa hayo mawazo ya mwanasiasa huyo ni sahihi, na kama yakifutwa kwa makini, basi yatawasogeza watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine yenye maendeleo zaidi.
Wakati mwingine, mwanasiasa mwenyewe hana uhakika kama yupo sahihi, lakini anajaribu kuwavutia watu tu ili afanikishe malengo yake.
Miezi kadhaa imepita tangu watu fulani waliposema walikuwa ni kama mfano wa wanyama wanaotambaa na wenye damu baridi, wakaueleza uma ya kuwa wamebadili safu yao na kuanza vita na mafisadi kwa mfumo wa kujivua makoti ya zamani na kubakia na makoti mapya.
Lakini .... naona sina kumbukumbu kama walivua makoti au walinyofoa mifuniko ya makoti yao tu.
Sasa tunasikia tena wamebadili safu na wamekuja na usemi ule ule wa vita tena ile ile.....
Kwa hiyo tusubiri tena mwaka 2014 wakibadili safu za serikali za vijiji, tena tutasikia nini tena!! aaah
Kwangu, nafikiri hakuna sababu ya kuendeea kuwapa nafasi watu wenye ahadi tuuuu au vipi!
Ninachukia siasa za ahadi hewa! Tubadilike alaaa!!
Sunday, 18 November 2012
Thursday, 8 November 2012
Romney: Your Time just Collapsed in the last minute
Mitt Romney .... May be your time is not yet
Obama has won re election by scooping minority, women and youths votes.
From African-American he scooped 93%, 71% of Latinos, and Asian origin individuals.
Apart from this, his party obtained 2 extra senate seats, these are Massachusets and Indiana.
Overall he got 303 electoral votes while Romney obtained 206 electoral votes.
Good luck Americans!

Monday, 29 October 2012
Sunday, 30 September 2012
Adha na Raha ya Kazi ya Huduma kwa Jamii
Kazi zinahusiana na kutoa huduma kwa jamii zina raha zake na karaha zake.
Kazi hizi ni kama vile za siasa, sekta ya afya, polisi, huduma za hoteli na migahawa, benki na kadhalika.
Wakati wote unahitaji kuwa mchangamfu na unayejali.
Hata pale anapokuja mtumishi wako wa nyumbani, ule ukali wako wooote, unayeyuka anapokuja ofisini kwako kwa ajili ya kupata huduma.
Lakini sina hakika kama watu wote wanakuwa hivi....
Nilikuwa nawatakia wikend njema tu!

Wednesday, 12 September 2012
Mfanyakazi Takukuru - Ngara Ajiua kwa Kujipiga Risasi
Mfanyakazi mmoja wa TAKUKURU wilaya ya Ngara, siku chache zilizopita alijiftyatulia risasi na kufa papo hapo kwa sababu ambazo bado hazijafahamika.
Mfanyakazi huyo kazi yake kubwa ilkuwa ni ya masuala ya usalama na utunzaji wa zana za moto (silaha), ambaye pia ni mwenyeji wa mkoa mmojawapo wa nyanda za juu kusini magharibi mwa Tanzania, ambapo mkoa huo hapo awali ulikuwa na sifa ya wenyeji wake kujiua pale wanapoudhiwa kupita kiasi.
Chanzo cha mtu huyo kufikia uamuzi mgumu kama huo hakijajulikana wazi, japo inasemekana alitakiwa kutoka kwenye kikao ambacho kinahisiwa kilitakiwa kukaa na kumjadili yeye.
Alipotoka nje ya kikao, muda mfupi baadaye ulisikika mlio wa risasi, jambo ambalo lilizua taharuki kutoka kwa wajumbe waliokuwa kwenye kikao cha kazi na kuwafanya wakimbie hovyo huku wakisigana kupita kwa kasi ya ajabu kwenye mlango wa kuingilia kwenye chumba hicho cha mkutano.
Habari zaidi zinadai ya kuwa funguo za chumba cha silaha alikuwa amekwisha kuzikabidhi kwa mamlaka husika kazini kwake, na kuna hisia labda alikuwa amekwisha itoa silaha iiyomuua, au alikuwa janja na kutoa nakala ya ufunguo wa chumba cha kuhifadhia silaha za moto.

Saturday, 8 September 2012
Friday, 31 August 2012
UEFA Champions League 2012 /13 Groups
Group A
FC Porto (Portugal)
Dynamo Kiev (Ukraine)
Paris Saint-Germain (France)
Dinamo Zagreb (Croatia)
Group B
Arsenal (England)
Schalke 04 (Germany)
Olympiacos (Greece)
Montpellier (France)
Group C
AC Milan (Italy)
Zenit Saint Petersburg (Russia)
Anderlecht (Belgium)
Malaga (Spain)
Group D
Real Madrid (Spain)
Manchester City (England)
Ajax Amsterdam (Netherlands)
Borussia Dortmund (Germany)
Group E
Chelsea (England)
Shakhtar Donetsk (Ukraine)
Juventus (Italy)
Nordsjaelland (Denmark)
Group F
Bayern Munich (Germany)
Valencia (Spain)
Lille (France)
BATE Borisov (Belarus)
Group G
Barcelona (Spain)
Benfica (Portugal)
Spartak Moscow (Russia)
Celtic (Scotland)
Group H
Manchester United (England)
SC Braga (Portugal)
Galatasaray (Turkey)
CFR-Cluj (Romania)
Group E
Thursday, 30 August 2012
Rwanda: Makahaba wauawa na Watu Wasiojulikana
Kumezuka wimbi la mauaji ya wasichana Nchini Rwanda. Mpaka sasa wanaohusika na mauaji hayo hawajajulikana.
Mauaji hayo yanawalenga wasichana makahaba. Kwa mwezi huu wa Agosti pekee, wasichana 15 wamekwishauawa kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na kukatwa katwa kwa vitu vya ncha kali au kunyongwa.
Jana mchana kuna habari ya kuwa wasichana watatu waliuawa kwa kunyongwa kwenye nyumba moja ambayo ipo sehemu ya makazi ya watu wengi. Mauaji hayo yanahisiwa kufanywa nyakati za mchana.
Hata majirani walistaajabu kupata habari za vifo hivyo, bila wao kusikia au kuhisi chochote.
Kwa sasa, katika nchi ya Rwanda, masuala ya kuendesha shughuli za ukahaba ni kosa la jinai.
Hakuna shaka mauaji haya hayahusiani na vyombo vya dola, bali kuna uwezekano yanaendeshwa na watu wanaochukia shughuli za ukahaba.

Subscribe to:
Posts (Atom)