Huu Mgogoro au vurugu za Zanzibar ni kweli unahusu kudai majadiliano ya muungano au una malengo tofauti?
Sijaelewa kwa nini zinazoshambuliwa zaidi ni taasis za kidini!
Nawaza kwa maandishi tu.
Nawatakia Jumanne njema
Tuesday, 29 May 2012
Monday, 28 May 2012
Pale Unapokutana na Mtu Usiyemtarajia!
Wiki hii nilipata mwaliko maalumu wa chakula cha usiku kutoka kwa mtu ambaye hatufahamiani.
Habari hizi nililetewa na mtu ambaye tumekwisha fanya kazi pamoja kama mara 3 hivi katika kituo cha kulelea watoto yatima na wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na wenye mtindio wa ubongo.
Katika kituo hiki cha kulelea watoto yatima, nilikataa kupokea malipo yoyote kutoka kwa huyu mtu aliyeniomba nije kuwapima watoto hao na kutoa ushauri wa kitaalam. Niliamua kufanya kazi ya ujuzi wangu kwa kujitolea kutokana na mguso nilioupata baada ya kuwaona watoto wenyewe, kwani hapo awali sikudokezwa ya kuwa kuna watoto wenye ulemavu na wengine wana mtindio wa ubongo.
Historia niliyoipata ya mahangaiko aliyopata mtu huyu labda nimuite msamaria mwema, alijitahidi kutafuta wataalamu kwa miezi zaidi ya mitatu na walikuwa wanatoa miadi ya kuja lakini baadaye wanajitoa kwa sababu mbalimbali. Kama alivyoniambia, jiwe lake la mwisho ndio hilo alilonirushia mimi, na hakutegemea kama angepata mtu kwani alikuwa anahitaji watoto waonwe kabla ya mwisho wa mwezi huu ili kuagiza chochote kitakachowasaidia.
Kwangu bila kujua historia hiyo, aliponipigia simu baada ya kupata taarifa zangu kupitia ofisi za ubalozi wa Marekani hapa Kigali, nilimpa siku ya kwenda kuwaona kwani nilikuwa nina ratiba ngumu sana kwa wiki hiyo. Ilibidi nivunje ratiba yangu ya kazi kwa muda japo kwa shingo upande. Siku na saa niliyoahidi nilifika kwa muda tuliopanga hata yeye hakuwa na imani ya kwamba nitafika kutokana na uzoefu alioupata hapo awali.
Kuhusu mwaliko wa chakula cha usiku, ambao ulifanyika Jumamosi tarehe 26 May 2012 .....Nilikubali kufika kwenye hoteli ambapo nilijulishwa kuwa wameandaa meza maalum kwani ilitolewa oda maalum tangu asubuhi kwa ajili ya chakula hicho. Nilikutana na mtu huyo ambaye ni Mzungu na raia wa Marekani. Alikuja na mkewe ambaye ndio yule nilikutana naye kwenye shughuli ya kuona watoto.
Mwenyeji wangu na mkewe walionekana waungwana sana na wenye heshima. Hata walivyonipokea walionyesha kujali na kuwa waungwana, sikuwa nimezoea hali hii ya kuongozwa na kufunguliwa milango nk. Pia, wahudumu kuwepo muda wote na kubadili hiki na kile, kama vile tupo kwenye dhifa fulani, kumbe tupo watatu tu!
Tuliongea mambo mengi ya binafsi na maisha yetu hapa Rwanda. Tuligusia kidogo mambo ya uchumi na siasa. Siku ilikuwa nzuri na chakula kizuri pia.
Baadaye nilifahamishwa ya kuwa mwenyeji wangu alikuwa ni mwakilishi mkaazi wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) nchini Rwanda! Na alipata habari zangu akapenda kukutana nami kwa ajili ya mazungumzo ya kawaida na kufahamiana. Japo mimi sina taaluma na mambo ya fedha wala uchumi, na shughuli zangu hazihusu masuala hayo. …… Bado ninatafakari ….. kwa nini alipenda kukutana nami, wakati shughuli zilizonikutanisha na watu wengine, taasisi yake haishughuliki moja kwa moja katika uendeshaji wake.
Nimependa tu kuwasiliana nawe msomaji, ujue ya kuwa kuitika wito ni bora, japo unaweza kuichuja habari ulioitiwa au kuikataa.

Friday, 25 May 2012
Jihadhari na Bidhaa Kutoka China
Kwa siku nyingi kumekuwa na malalamiko kutoka nchi zinazoendelea kuhusiana na uduni wa bidhaa kutoka China.
Serikali ya China ilikuwa inajitetea na kusema inaudha bidhaa zake kutokana na mahitaji ya wateja, maana yake nchi zinazoendelea zilikuwa zina agiza bidhaa za bei nafuu lakini zikiwa na ubora duni.
Serikali ya Tanzania kupitia mamlaka zake, ilikuwa inazikamata bidhaa bandia na kuziteketeza. Jitihada hizi hazijaweza kuzimaliza bidhaa bandia au feki au zenye ubora wa hali ya chini.
Wiki iliyopita, Serikali ya Marekani ililaumu China kwa kuiuzia vifaa vya ndege za kivita ambavyo takribani asilimia 60 ya vifaa vilivyotumika kutengeneza ndege za kijeshi, vilikuja kugundulika kuwa vilikuwa chini ya kiwango.
Uchunguzi uliofanyika na taasisi za Marekani kwenye bidhaa nyingine zilizoingizwa nchini humo zikiwamo nguo, baiskeli nk umebaini ya kuwa bado wanatengeneza na kuzipeleka bidhaa bandia zenye ubora hafifu wakati mwingine kwa asilimia 90 ya bidhaa zote wanazoziingiza Marekani, japo wanabandika alama au lebo sahihi. Watu wamejikuta wakinunua lebo sahihi huku bidhaa ikiwa bandia.
Baadhi ya taasisi zimeshindwa kuyafunga maduka au kuteketeza bidhaa zilizouziwa bidhaa bandia kutoka China kwani wanahofia kuwa kuna mamilioni ya watu watapoteza ajira wakati kuna kiu kubwa ya ajira kwa watu wengi!
Habari zipo nyingi, lakini unaweza kusoma mojawapo hapa

Sunday, 20 May 2012
Chelsea: New European Champions - 2012
Drogba was the man of the day for Chelsea.
He scored an equiliser goal in 88th minute and send the match into extra time.
He gave penalty to Bayern Munich during the extra time while he was trying to defend the goal. But Arjen Robben spot kick was denied by Chelsea goal-keeper Cech.
He scored the the last penalt kick which earn Chelsea the European Champion trophy for the first time in their history. They beat Bayern Munich by 4 - 3 penalties.
Some statistics: Bayern Munich vs Chelsea
Total Shots 34 9
Corners 20 1
Fouls committed 11 26
Congratulations Chelsea!

Sunday, 13 May 2012
Simba yatolewa Na Al Ahly Shandy kwa Penati 9 - 8
Mabingwa wa mpira wa Miguu Tanzania Simba ya Dar es salaam, usiku wa tarehe 13 May 2012 imeyaaga mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufungwa magoli 3 - 0 na Al-Ahly Shandy ya Sudan kwenye muda wa kawaida.
Magoli yote hayo yalifungwa katika kipindi cha pili, la kwanza likiwa dakika ya kwanza kipindi cha pili, yakifuatiwa na jingine dakika 3 baadaye. La tatu lilifungwa baada ya dakika 10 baada ya goli la pili kwa uzembe wa Victor Costa kwa kutokuwa makini na utoaji wa pasi na hivyo kupoteza mpira huo uliomfikia mchezaji wa Al-Ahly Shandy aliyefunga kwa urahisi. Mwisho wa dakika 90 mabao yalikuwa 3 - 0 dhidi ya Simba, na hivyo kufanya kuwe na jumla ya mabao 3 - 3.
Mshindi alipatikana kwa njia ya penati ambapo jumla ya penati 10 zilipigwa. Juma Kaseja alishindwa kufunga penati ya mwisho kwa Simba na hivyo kuzidiwa bao moja na Al-Ahly Shandy
Simba wanatarajiwa kurudi Dar es Salaam Jumatatu, ili waanze kuganga mashindano mengine.
Man City Made it ... Since 1968
English Premier league 2011/12 season has ended with a dramatic win for Man City over QPR after being trailling by 2 - 1 until the injury time. The heroes were Dzeko and Aguero who scored two vital goals on stoppage time to lift up Man City to the top spot of English Premier League.
It was a great moment for Man City fans who had been seated on hot coal throughout the game.
Manchester United came second after the narrow win 1 - 0 over Sunderland, just beaten by goal difference with arch-rival and Premier Champions, Manchester city. Arsenal came out third when they won against West Bromwich Albion by 3 - 2 goals, and Tottenham clinch the last post for Champions League
Both Arsenal and Manchester united have a good record for Champions League qualiffication. However, for this year they both finished without any title.
Wednesday, 9 May 2012
Wakuu wapya wa Wilaya Tanzania Bara
Ifuatayo ndio orodha ya wakuu wapya wa wilaya Tanzania Bara kama walvyiotajwa leo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Idadi ya wakuu wa wilaya walioachwa ni 51.
Wakuu wa wilaya wapya na sehemu walizopangiwa ni:-
1. Novatus Makunga - Hai
2. Mboni M. Mgaza - Mkinga
3. Hanifa M. Selungu - Sikonge
4. Christine S. Mndeme - Hanang
5. Shaibu I. Ndemanga - Mwanga
6. Chrispin T. Meela - Rungwe
7. Dr. Nasoro Ali Hamidi - Lindi
8. Farida S. Mgomi - Masasi
9. Jeremba D. Munasa - Arumeru
10. Majid Hemed Mwanga - Lushoto
11 Mrisho Gambo - Korogwe
12. Elias C. J. Tarimo - Kilosa
13. Alfred E. Msovella - Kiteto
14. Dkt. Leticia M. Warioba - Iringa
15. Dkt. Michael Yunia Kadeghe - Mbozi
16. Mrs. Karen Yunus - Sengerema
17. Hassan E. Masala - Kilombero
18. Bituni A. Msangi - Nzega
19. Ephraem Mfingi Mmbaga - Liwale
20. Antony J. Mtaka - Mvomero
21. Herman Clement Kapufi - Same
22. Magareth Esther Malenga - Kyela
23. Chande Bakari Nalicho - Tunduru
24. Fatuma H. Toufiq - Manyoni
25. Seleman Liwowa - Kilindi
26. Josephine R. Matiro - Makete
27. Gerald J. Guninita - Kilolo
28. Senyi S. Ngaga - Mbinga
29. Mary Tesha - Ukerewe
30. Rodrick Mpogolo - Chato
31. Christopher Magala - Newala
32. Paza T. Mwamlima - Mpanda
33. Richard Mbeho - Biharamulo
34. Jacqueline Liana - Magu
35. Joshua Mirumbe - Bunda
36. Constantine J. Kanyasu - Ngara
37. Yahya E. Nawanda - Iramba
38. Ulega H. Abadallah - Kilwa
39. Paul Mzindakaya - Busega (mpya)
40. Festo Kiswaga - Nanyumbu
41. Wilman Kapenjama Ndile - Mtwara
42. Joseph Joseph Mkirikiti - Songea
43. Ponsiano Nyami - Tandahimba
44. Elibariki Immanuel Kingu - Kisarawe
45. Suleiman O. Kumchaya - Tabora
46. Dkt. Charles O. F. Mlingwa - Siha
47. Manju Msambya - Ikungi (mpya)
48. Omar S. Kwaangw’ - Kondoa
49. Venance M. Mwamoto - Kibondo
50. Benson Mpesya - Kahama
51. Daudi Felix Ntibenda - Karatu
52. Ramadhani A. Maneno - Kigoma
53. Sauda S. Mtondoo - Rufiji
54. Gulamhusein Kifu - Mbarali
55. Esterina Kilasi - Wanging’ombe (mpya)
56. Subira Mgalu - Muheza
57. Martha Umbula - Kongwa
58. Rosemary Kirigini - Meatu
59. Agness Hokororo - Ruangwa
60. Regina Chonjo - Nachingwea
61. Ahmed R. Kipozi - Bagamoyo
62. Wilson Elisha Nkhambaku - Kishapu
63. Amani K. Mwenegoha - Bukombe
64. Hafsa M. Mtasiwa - Pangani
65. Rosemary Staki Senyamule - Ileje
66. Selemani Mzee Selemani - Kwimba
67. Lt. Col. Ngemela Lubinga - Mlele (Mpya)
68. Iddi Kimanta - Nkasi
69. Muhingo Rweyemamu - Handeni
70. Lucy Mayenga - Uyui

Tuesday, 8 May 2012
Makinda: Tanzania Haijawa Tayari Kuridhia Kuondolewa kwa Masharti ya Uhamiaji EAC
Mkutano wa viongozi wa mabunge (National assembly speakers) ya nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaokutana jijini Kigali, Rwanda walikuwa na mjadala mkali unaohusu kufungulia mipaka na kelegeza masharti ya uhamiaji kati ya nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Habari zinadai ya kuwa mashambulizi mengi yalielekezwa kwa Tanzania kwani bado haijaridhia kufungulia mipaka yake kama nchi nyingine zinavyopenda kuharakisha mkataba huu.
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda alisema kwa sasa Tanzania haipo tayari kufanya hivyo kwa kuwa wananchi wa Tanzania wanatakiwa kuulizwa kwanza kama wapo tayari kufanya hivyo ukizingatia ina idadi kubwa ya watu kuliko nchi zote za Afrika Mashariki. Pia aliongeza kusema ya kuwa kumekuwa na wahamiaji haramu wengi wanaoingia Tanzania kutoka nchi mbalimbali hata zilizo nje ya Afrika mashariki ambao huleta vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani ndani ya Tanzania. Kwa hiyo kuna haja ya kudhibiti hilo kwanza.
Kingine alichoongeza Mama Makinda, ni kuwa Tanzania haina vitambulisho vya taifa, na kwa sasa iko kwenye mpango wa kuvitoa kwa wananchi, na hatarajii zoezi hilo litakwisha mapema, labda litachukua zaidi ya miaka miwili kutoka sasa.

Subscribe to:
Posts (Atom)