Member of EVRS

Sunday, 25 March 2012

Monday, 19 March 2012

Wednesday, 14 March 2012

Jiolojia: Afrika kugawanyika na Kuwa Mabara Mawili!

Wanasayansi wa jeolojia ambao wamekuwa wanafanya utafiti wa namna bahari inavyotokea katikati ya nchi kavu hivi karibuni wamegundua mvutano mkubwa wa sumaku katika bonde la Afar nchini Ethiopia. 
 
Mvutano huu wa sumaku ndio unaosemekana kuwa chanzo cha mkondo wa bahari kutokea mahali. Na mara nyingi hufanya kuwa tofauti ya nguvu za kisumaku katika tabaka la udongo, hii ni kutokana na miamba moto kusogea juu karibu na uso wa ardhi na kisha kupoa. Inapotokea mvutano wa kisumaku kutokea, miamba hii huanza kutoa nguvu za kisumaku kuelekea upande mwingine kuliko ilivyokuwa awali na hivyo kukinzana na miamba ya awali, na hivyo kuchochea miamba kusigana na kuachanana hivyo kutengeneza mkondo mpya wa bahari. 
 
Mara nyingi mivutano kama hii huonekana kwenye maeneo ya bahari kuu. 
  
Iwapo msukumo huu wa kisumaku utaendelea, basi kuna uwezekano wa bara la Afrika kugawanyika katika sehemu mbili zikitengwa na bahari. 
  
Ili kuweza kuwa na ufa inakadiriwa kuwa itaweza kupita miaka kama milioni 2, na kuweza kuacha nafasi ya mkondo wa bahari, inakadiriwa itahitajika kama miaka milioni 2 mingine ipite.  
Kwa hiyo watakaoshuhudia bahari hiyo, ni wale watakaokuwa wanaishi duniani mika akam milioni 4 ijayo.
  
Mimi sina utaalamu wa aina yoyote ya jiolojia, Kama unayaamini haya, basi habari ndiyo hiyo, inapatikana hapa pia 

Sunday, 4 March 2012

Chelsea: Yamtimua Kocha Wake Andre Villas-Boas

Klabu ya mpira wa miguu ya Chelsea ya jijini London, leo imemfutia kazi ya kuifunza timu hiyo kocha Andre Villas-Boas baada ya kutetereka katika michezo ya ligi kuu ya England na pia mashindano ya Ubingwa wa ulaya. 
  
Kufuatia kupoteza mechi ya jana dhidi ya timu ya West Bromwich Albion kwa bao 1 - 0 wakiwa ugenini kulihamasisha uamuzi wa uongozi wa Chelsea kumuondoa kocha huyo mwenye umri wa miaka 34.
 
Kupoteza mechi hiyo ya jana kuliweka rekodi ya Chelsea kushinda mechi 3 tu kati ya 12 za mwisho za ligi kuu ilizocheza. 
 
Andre amedumu kwa siku 257 tu ndani ya Chelsea tangu alipoanza kazi ya kuifundisha Chelsea kuanzia tarehe 22 Juni 2011. Katika kipindi chote alichokuwa Chelsea, kocha huyu amekuwa akidaiwa ya kuwa alikuwa na migongano na wachezaji "wazee" ndani ya Chelsea, lakini haijathibitishwa ya kuwa ndio chanzo cha Chelsea kufanya vibaya msimu huu.
 
Kwa muda wa siku 10 zijazo, Chelsea itakuwa na kazi kubwa ya kuishinda timu ya Napoli ya Italia katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kupoteza mechi ya awali nchini Italia kwa kufungwa magoli 3 - 1.
Kabla ya hapo watalazimika kucheza mechi ya ugenini dhidi ya timu ya Birmingham kwenye mashindano ya kushindania kutwaa Kombe la chama cha soka cha Uingereza (FA Cup). Itakumbukwa ya kuwa mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge, timu hizo zilitoka sare ya bao 1 - 1 huku Chelsea ikitoka nyuma na kusawazisha bao hilo. Kwa sasa, timu ya Birmingham ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo.

Saturday, 18 February 2012

Adimiko la Muda

Kijiwe hiki kimeamua ya kuwa kitakuwa kimya hapa na pale wakati wadau watakapokuwa wanahama hama ili kubadili mazingira na kuweka mambo vichwani sawa. 
  
Kitakuwa kinajitokeza pale muda utakaporuhusu.  
   
Kama kawaida tupo wote!

Friday, 17 February 2012

Waume wa Maswa Watakiwa Kupewa Elimu ya Uzazi

BAADHI ya wanawake wilayani Maswa, Shinyanga, wameomba waume zao washirikishwe katika elimu ya afya ya uzazi ili waweze kufahamu matatizo yanayowakumba pindi wanapokuwa wajawazito.
Ombi hilo lilitolewa juzi katika kijiji cha Gulungwashi kata ya Malampaka mbele ya Ofisa Utafiti wa shirika la Utu Mwanamke, Catherine Kamugumiya, wakati wakibainisha matatizo yanayowakabili kipindi cha ujauzito na kujifungua huku waume zao wakiwa mbali na matatizo hayo.
“Matatizo mengi ya uzazi yanayotukumba sisi wanawake wengi yanatokana na waume zetu kukosa elimu ya afya ya uzazi ukizingatia hawa ndiyo wasaidizi wetu wa karibu pindi tunapopata matatizo haya,” alisema Leah Nghumbi.

Pata habari kamili kupitia Tanzania daima hapa

Wednesday, 15 February 2012

Matangazo katika Nyumba Za Kufikia Wageni




Hii ni mikakati ya kupambana na tabia zisizofaa kwa Jamii za Kitanzania. Hasa kipengele namba 8 na 12!

Tuesday, 14 February 2012

Valentine's Day 2012!


People busy buying valentine's day gifts at shopping points as seen yesterday at Kigali, Rwanda


Just be happy and Love all !!!