Umh! I am on Christmas and New Year Vacation.
Visiting blog is altered due to here and there travelling.
I will keep posting whenever I get time.
I wish you a Happy New Year 2011
Wednesday, 29 December 2010
Friday, 24 December 2010
Tanesco! Bado Kabisa!
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kwa hivi karibuni limeanza kututumka na kutaka kuonyesha kuwa linawajali na kuwaheshimu wateja wake na kuthamini malipo yao kuwa ndio uha wa Tanesco (kwani ndio linawafanya watendaji waweze kwenda haja).
Kumekuwa na vipindi vingi vya kwenye radio na runinga wakijielezea mikakati yao, kujibu maswali ya wasikilizaji na watazamaji na pia kutoa ushauri kwa wenye malalamiko wapi wataweza kusikilizwa.
Hata siku ya tarehe 23 Desemba 2010, waziri wa nishati na madini Mh. Ngeleja akiwa na watendaji wa Tanesco, alikuwa akitoa maelezo na kujibu maswali ya wasikilizaji/watazamaji moja kwa moja (live bila chenga).
Mbali ya juhudi za uongozi wa juu kujaribu kulisafisha shirika hili la ugavi wa umeme, bado watendaji wa ngazi za chini yao, wana roho zilizosheheni kutu, utukutu wa akili au makusudi na kutowajibika.
Kuna sehemu fulani huko manispaa ya Ilala kuna nguzo imeoza na kuegeme ukuta nyumba kwa zaidi ya miaka 3 sasa. Wenye nyumba walishapiga kelele weee mpaka wakamwachia Mungu awalinde hizo nyaya zisijeangukia watu hususan watoto, basi ndio ikawa mauti tena.
Mpita njia waweza kuona nguzo hiyo ikiwa imeegemea ukuta, na kwa hapo chini utaona ule waya unaoshikilia nguzo ikae wima ukiwa umelegea kabisa, kuashiria ya kuwa hauna kazi tena kama ilivyokusudiwa!
Picha hii chini inaonyesha nguzo ikiwa imekwisha kabisa na kugeuka mahali pa ndege kujikinga na jua la Dar es salaam!
Na hii picha juu ndio hali halisi ya nyaya za umeme zikiwa zimeshuka chini kabisa chini ya usawa wa mabati ya nyumba! Kinachoshangaza, wiki chache zilizopita, watu wa Tanesco walikuja kumuunganishia umeme mteja mpya, na wakaweka waya kutoka kwenye nguzo hiyo hiyo iliyooza, na walipotaarifiwa kuhusu ubovu wa mlingoti huo, waliuangalia na kusema wanaenda kutoa taarifa ofisini, na kwa sasa inakaribia miezi 2 na hakuna taarifa wala mtu aliyekuja kuona.
Watendaji wa kweli walipotaarifiwa, wakawapa maelekezo walalamikaji mahali pa kwenda na namba za simu, sasa sijui nicheke au... mhusika alipopatikana kwa simu, alisema yupo likizo na akatoa namba nyingine ya mtu ambaye kwa zaidi ya wiki amefunga simu, na watu wakamshauri mlalamikaji ati asubiri sikukuu zipite ndipo akaulizie tena!!!!!
Hivi hizo nyaya za umeme na nguzo zinajua sikukuuu hizo ambazo Tanesco wanasubiri ziishe kwanza!
Na hao wafanyakazi watafungaje line mpya kwenye nguzo wanayoiona imeoza?!
Likitokea janga ... ni nani wa kulaumiwa.
Hakika watendaji wabovu wa Tanesco wanastahili kuongozwa na mtu kama Stalin :-(
Tuesday, 21 December 2010
Hukumu ya BAE SYSTEMS Kutolewa Leo
Hukumu kesi ya shirika kubwa la kuuza silaha la Uingereza (BAE Systems) itatolewa kesho na Jaji Bean anayesikiliza madai ya kampuni hiyo kujihusisha na rushwa kubwa kwa kuiuzia Tanzania radar ya kijeshi ambayo iliigharimu nchi maskini ya Tanzania zaidi pauni za Uingereza milioni 28 ( Zaidi ya sh.billioni 70 za kitanzania)
Hakimu huyo aliihoji kampuni hiyo kuhusu madai ya kumlipa mfanyabiashara Sailesh Vithlani kiasi cha kama pauni millioni 7.7, katika kujitetea kampuni hiyo ilidai ilitoa pesa kumpa Vithlani kwani walimtumia kama papa mdogo kupenyeza ili waweze kushinda zabuni ya kuiuzia Tanzania rada hiyo kwa bei ya kuruka.
Kampuni ilikiri kuwa na kosa dogo la kuweka vizuri kumbukumbu za mahesabu kwa kudai walimlipa Vithlani kama mshauri wa kiufundi wakati Vithlani mwenyewe hakuwa na ujuzi wowote katika masuala hayo ya ununuzi wa rada.
Jaji hakuridhika na maelezo hayo, na akaendelea kusisistiza kuna kila dalili ya rushwa kwani alihoji kwa nini zaidi ya 97% ya malipo ilipitia kwenye mikono ya Vithlani!, kiasi kwamba alitaka kutoa uamuzi wa kuita mashahidi kueleza ni vipi pesa alizopewa Vithlani zilivyotumika kabla ya kutoa hukumu yake, lakini baadaye alibadili mawazo yake na kuahidi kutoa ya hukumu dhidi ya BAE System leo siku ya Jumanne.
Hapo awali, kampuni hii ilikiri kuwa na makosa ya kuweka vibaya kumbukumbu za pesa, na ilikubali kulipa pauni milioni 3 kama fidia kwa Tanzania na pesa hizo kutumika nchini Tanzania kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Lakini ikawa inasisitiza haikutoa mlungula wowote.
Pata maelezo zaidi kwa mwanzilishi wa mjadala huu wa uuzwaji wa rada hii kwa bei isiyo na tija

Monday, 20 December 2010
WikiLeaks Cable Hit Tanzania
Today I was reading Subi's Wavuti and came accross this astonishing news about radar scam!
Quoted ......The Tanzanian prosecutor, Edward Hoseah, investigating worldwide misconduct by BAE, Britain's biggest arms company, confided to US diplomats that "his life may be in danger"...
Hoseah met a US diplomat, Purnell Delly, in Dar es Salaam in July 2007, and claimed (unrealistically it turned out) he would be able to prosecute guilty individuals in the BAE case. The US cable reports: "He called the deal 'dirty' and said it involved officials from the Ministry of Defence and at least one or two senior level military officers."
Hoseah spoke gloomily about the prospects for Tanzania's anti-corruption struggle and his original hopes to prosecute the "big fish" of corruption.
"He told us point blank... that cases against the prime minister or the president were off the table ..." The cable then details allegations against former leaders and their inner circles, saying they would be "untouchable".................
Today, is the beginning of the case related to BAE fraud on radar scam. More terrible news are going to be revealed out ....
The Guardian (UK) has more astonishing news

Friday, 17 December 2010
Enjoy your Weekend!
Hi Guys, I am still with you.
But, I wish christmas will be ten weeks ahead, so that this working under pressure to beat the deadlines will be kept out of our mind and order.
I wish you the nice weekend for those who will have the really weekend.

Wednesday, 15 December 2010
Homa ya Harusi ya Prince William Yazidi Kupanda
Baadhi ya makampuni ya kutengeneza zawadi yameanza kuchangamkia tenda ya kutengeneza zawadi ya Harusi ya mjukuu wa malkia wa Uingereza Prince William ambaye anatarajjia kufunga ndoa na Kate Midleton mwishoni mwa mwezi Aprili 2011.
Kampuni hizo zipo Uingereza na China.
Wamiliki wameanza kutengeneza vito vya thamani kama pete na vyombo vingine vikiwa na picha ya mtoto huyo wa kifalme na mchumba wake, kwani wanatarajia soko litakuwa kubwa sana hapo harusi itakapokuwa inakaribia.
Kampuni moja ya China imeanza kutengeneza pete mfano wa ile ya uchumba ambayo Kate amejipatia. Pete hiyo ambayo imetengenezwa kwa almasi za rangi tofauti tofauti ikizunguka kito cha rangi ya sapphire ilikuwa ya Diana. William alisema hakutaka kabisa marehemu Mama yake apitwe na tukio lolote la harusi hiyo, ndio maana alikubali mchumba wake avikwe pete ambayo ilikuwa ya uchumba ya mama yake.
Wachina wamepata haki ya kutengeneza mfano wa pete hiyo, na kwa yeyote anayetaka kununua, Soko lipo wazi sasa.
Harusi hiyo ambayo itaonyeswa moja kwa moja na vyombo vya runinga mbalimbali inatarajiwa kuvunja rekodi ya harusi kuangaliwa na watu wengi duniani.
Gonga hapa kupata habari zaidi

Monday, 13 December 2010
Gwiji la Muziki Remmy Mtoro Ongala Afariki Dunia
Mwananmziki mkongwe na maarufu nchini Tanzania, Ramadhani Mtoro Ongala au maarufu kama Dokta Remmy amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Remmy alikuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kisukari ambao ulisababishwa alazwe mara kadhaa hospitalini ikiwa ni pamoja na hospitali ya taifa ya Muhimbili. Inasemekana amefariki kwa matatizo hayo hayo ya kisukari.
Remmy atakumbukwa kwa mengi ikiwa ni pamoja na kuwa mshindi wa pili kwa sura mbaya Tanzania japo alilalamika ya kuwa kaonewa kwani aliamini ya kuwa yeye ana sura mbaya kuliko watu wote waliokuwa wanaishi Tanzania wakati huo!!!!!
Pia kuna nyimbo kadhaa alizoimba ambazo watu watatzikumbuka ikiwa ni pamoja na wimbo wa KIFO.
Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi

Saturday, 11 December 2010
Tanzania Bara Yaingia Fainali ya CECAFA Tusker Challenge Cup 2010
Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) hapo juu wakishangilia ushindi, jana ilifanikiwa kuingia fainali ya kombe la CECAFA baada ya kuwafunga timu ya Uganda (The Cranes) kwa mikwaju ya penati 5 - 4
Kipa namba moja wa Kilimanjaro Stars, Juma Kaseja kama anavyoonekana hapo juu akiiokoa penati moja ya waganda na hivyo kuifanya Tanzania Bara kuingia fainali.
Fainali itakuwa kesho, ambapo Tanzania Bara itapambana na timu ya Ivory Coast. Hata hivyo ni lazima kombe libaki Tanzania hata kama Ivory Coast itashinda, kwani timu hii ya Afrika Magharibi ilialikwa tu kupasha moto mashindano, na sheria za CECAFA timu mualikwa huwa haipewi kikombe, isipokuwa inapewa zawadi iliyopangwa kwa mshindi wa kwanza, na kikombe huchukuliwa na nchi mwanachama aliyeshika nafasi ya juu.
Kwa maana hiyo, Kilimanjaro Stars ndiyo itakayopewa kombe hilo kwa matokeo ya aina yoyote.
Tuna imani Tanzania Bara itashinda na kuchukua kombe hilo.
Picha kutoka kwa michuzi

Subscribe to:
Posts (Atom)