Nilikuwa nikiangalia runinga leo asubuhi, nikapokea habari nzuri zinazohusu ujenzi wa barabara Tanzania.
Waziri wa ujenzi, Mhesh Pombe Magufuri akiwa na naibu waziri wake Prof Harrison Mwakyembe, jana walipokuwa wakiongea na watendaji wa wizara ya Ujenzi, alitoa muda wa mwezi mmoja kwa watendaji hao kujipanga na kumletea taarifa ya matarajio (projections) ya utendaji wao wa kazi kwa kipindi kijacho.
Magufuri aliyeonyesha ukali katika kauli zake, alikemea tabia ya usimamizi mbovu wa miradi ya serikali, na pia kutowajibika.
Mbali ya yote hayo, alielekea kushangaa ni kitu gani kinachoshindikana kujenga daraja la Kigamboni, akatolea mfano wa huko Uchina ambako aliona daraja lenye urefu wa km 26 likijengwa kwa miezi 14 tu. Alitoa rai kwa NSSF kujenga daraja hilo haraka iwezekanavyo, vinginevyo ataiomba benki kuu ya Tanzania kuidhinisha na kutoa pesa za ujenzi wa daraja hilo ili serikali isimamie. Kwa hapa naona ni neema kwa wakazi na wageni wanaotembelea Kigamboni ambao wamekuwa wana kilio hiki kwa muda mrefu sasa.
Cha kufurahisha zaidi, na iwapo kitakuwa cha vitendo, ni pale Magufuri aliposema uanze mpango na ujenzi wa madaraja ya juu ya kupitia magari (flyovers), kwani hakuna kinachoshindikana. Pia kuwaeleza wazi kutakuwa na ziara za kushtukiza kukagua kazi na miradi mbalimbali ya ujenzi, pale itakapokutwa kazi ya ujenzi inalegalega, basi mhandisi anayesimamia ajijue ya kuwa kibarua kimekwisha ota nyasi (Keshafutwa ajira).
Na mwisho aliwagawia watendaji wote ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 - 2015 ili waweze kufahamu ni nini serikali ya CCM inakusudia kutekeleza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kutoka sasa. Na ilani hizo walizigawa yeye mwenyewe na Mwakyembe kwa mikono yao wakimpa kila mtendaji pale alipokuwa amekaa, na sio watendaji kuzifuata kwenye meza kuu.
Mimi nasema, mwanzo huu unatia moyo, kwani tunawafahamu Magufuri na Mwakyembe ni watendaji wazuri na wasimamizi katika maslahi ya Taifa. Nawatakia kila la heri.
Monday, 29 November 2010
Friday, 26 November 2010
Have a nice weekend
I am running short of words......
This week was hectic ... busy.... whatever you call it..
Tomorrow, there is a community work here, no shop, market, bank, hotel, transport etc will be available from morning till mid day.
If you are going to airport, you..either go before 7.00 am or after mid day! I am very serious.
Wishing you a lovely weekend!! :-x

Thursday, 25 November 2010
Wednesday, 24 November 2010
Baraza la Mawaziri na Naibu Mawaziri Novemba 2010
Ofisi ya Rais:
Ofisi ya Makamu wa Rais
Wizara ya Fedha - Mustapha Mkulo
Naibu Gregory Teu na Pereira Ame Silima
Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Shamsi Vuai Nahodha
Naibu - Balozi Khamis Suedi Kagasheki
Wizara ya Katiba na Sheria - Celina Kombani
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa - Bernard Membe
Naibu Mahadhi Juma Mahadhi
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Dk Hussein Ali Mwinyi
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi - Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu - Benedict Ole Nangoro
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia - Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Prof. Anna Tibaijuka
Wizara ya Maliasili na Utalii - Ezekiel Maige
Wizara ya Nishati na Madini - William Mganga Ngeleja
Naibu - Adam Kigoma Malima
Wizara ya Ujenzi - Dr. John Pombe Magufuli
Wizara ya Uchukuzi - Omari Nundu
Wizara ya Viwanda na Biashara - Dr. Cyril Chami
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Dr. Shukuru Kawambwa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Dr. Haji Hussein Mpanda
Wizara ya Kazi na Ajira - Gaudensia Kabaka
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Sophia Simba
Wizara ya Habari, Vijana na Michezo - Emmanuel John Nchimbi
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Samuel John Sitta
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika - Prof. Jumanne Maghembe
Wizara ya Maji - Prof. Mark James Mwandosya
- Utawala Bora - Mathias Chikawe
- Mahusiano na Uratibu - Stephen Wassira
- Menejimenti ya Utumishi wa Umma - Hawa Ghasia
Ofisi ya Makamu wa Rais
- Muungano - Samia Suluhu
- Mazingira - Dr. Terezya Luoga Hovisa
- Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi
- Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu
- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Mkuchika
Wizara ya Fedha - Mustapha Mkulo
Naibu Gregory Teu na Pereira Ame Silima
Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Shamsi Vuai Nahodha
Naibu - Balozi Khamis Suedi Kagasheki
Wizara ya Katiba na Sheria - Celina Kombani
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa - Bernard Membe
Naibu Mahadhi Juma Mahadhi
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Dk Hussein Ali Mwinyi
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi - Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu - Benedict Ole Nangoro
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia - Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Naibu - Charles Kitwanga
Naibu - Goodluck Ole Madeye
Naibu - Adam Kigoma Malima
Wizara ya Ujenzi - Dr. John Pombe Magufuli
Naibu - Dr. Harrison Mwakyembe
Naibu - Athumani Mfutakamba
Naibu - Lazaro Nyalandu
Naibu - Philipo Mulugo
Naibu - Dr. Lucy Nkya
Naibu - Makongoro Mahanga
Naibu - Umi Ali Mwalimu
Naibu - Dr. Fenella Mukangara
Naibu - Dr. Abdallah Juma Abdallah
Naibu - Christopher Chiza
Naibu - Eng. Gerson Lwinge
Habari kutoka Ikulu Mawasiliano
Naomba Ushauri
Sehemu ninayoishi hapa Kigali, ina usalama wa hali ya juu, na patrol za polisi usiku zipo karibu muda wote!
Tarehe kama ya leo, yaani 24 Mei 2010, mfanyakazi wangu wa nyumbani (house boy) alirudi kutoka "kijijini" alipoenda kusalimia famlia yake, na aliporudi usiku nilishtukia tu yumo ndani ya ua, bila kufunguliwa geti.
Nilipomuuliza kaingia vipi, akasema alifungua mlango kwa ndani kupitia kidirisha cha ulinzi (Security window), kwa ujumla sikuamini amini. Siku iliyofuata niliporudi kutoka kazini nilikuta katoweka, baadaye niligundua upotevu wa fedha kutoka chumbani kwangu.
Habari ilifikishwa polisi, na hakuna kilichofanyika.
Kijana huyo alikuwa naaminiwa sana na kila mtu, lakini mimi tangu siku ya kwanza roho yangu ilimkataa. Japo familia yangu walielekea kumwamini na kumpenda. Sasa naona wamebadilika kuliko hata mimi!
Leo tarehe 24 Novemba( Sielewi kwa nini ni hii tarehe), miezi sita imetimia, wakati naingia gereji kujiandaa kuondoka kwenda kazini, niliona nyendo zisizo za kawaida kwenye kona ya gereji, nilipokaza macho zaidi nikaona macho ya blink hapo kwenye kona huku yakiwa yamefunikwa na mlango mbovu na viti chakavu. Nilipokamua macho zaidi, mara akaibuka kijana yule yule aliyekuwa mfanyakazi wangu. Akadai aliruka ukuta usiku kupata mahali pa kulala na kisha alikuwa anasubiri nikienda kazini, naye ajiondokee zake!
Kwa sababu kwa sasa naishi mwenyewe, nilitoka nje kuomba msaada wa mlinzi ili nimdhibiti, lakini alifanikiwa kwa muda kuchomoka na kukimbia, lakini weeee, watu wanajua kupiga mitama ama ngwara, hakufika mbali ndo hivyo tena akaibusu ardhi.
Baada ya kumfkisha polisi, akakiri alikwiba siku za nyuma. Na ni kweli aliruka ukuta kuingia ndani ya nyumba bila idhini yangu.
HUWEZI AMINI ALIHUKUMIWA KIFUNGO HAPO HAPO, na kwa sasa amekwisha anza kutumikia kifungo jela.
Hakuna kesi mahakamani wala kuhangaishana na kuleta ushahidi. kwani kila kitu kilikuwa hadharani.
Upekuzi wangu pale alipokuwa amejificha, nilikuta sanamu ya plastiki ya mnyama mwenye pembe 2 ambazo zipo sharp. Hiyo sanamu nilishawahi kuiona ndani ya nyumba miezi mingi wakati naingia, nikaitupilia jalalani. Pia sanamu hiyo nilipoikuta, siku za nyuma nilishawahi kukuta sanamu ya mtu aliyevishwa hirizi ya mbao!
Mimi ni mtu wa imani kidini na huwa sitetereki, kawaida yangu ni kuzichoma moto takataka kama hizo.
Bado najiuliza, kama nikimwona tena baada ya kifungo ndani ya himaya yangu nimfanye nini.

Sunday, 21 November 2010
Jumapili Njema
Jana modem yangu ya internet ilinigomea kabisa, nikashindwa kupata habari mpya.
Leo nimeshtukizwa na kuingia kazini tangu asubuhi mpakaaaa......
Hivyo nawatakia jumapili njema, na pia tuwaombee hao wanaume ambao wamezuka sasa na mtindo wa kuua familia zao kwa visu.
Kwani hivi karibuni huko Kilimanjaro mtu kaua mama yake mzazi na watoto wake wawili, juzi tu, huko Kenya kuna mtu kaua mke wake mjamzito na watoto wawili kwa visu tena, mmoja tu wa miaka 3 ndio alikimbia. Halafu tena wiki kadhaa zilizopita jamaa mmoja tena huko Marekani mwenye asili ya Afrika, aliua mke na watoto wake wawili kwa mtindo huo huo.
Bahati mbaya au nzuri kama utakavyochukulia wewe, wanaume hao wote nao walikufa aidha kwa kujiua au watu wenye hasira kali kuwamaliza!
Aaaah, nilishasahau, nilikuwa nataka kuwatakia jumapili njema tu!

Friday, 19 November 2010
USA 2012 Elections Fever start Rising Now
Sarah Palin, who was runner mate for 2008 Republican presidential candidate, has shown some interest for Republican presidential nomination for 2012 to challenge Democrats likely presidential candidate, Barack Obama.
The matter for running for presidential race is still under Palin family's discussion, but Palin's fans have started canvancing for her.
So far, Barack Obama has upper hand where still 55% have a positive minds towards him despite the hard economic challenges affecting the globe and his Government, while for Sarah Palin only 47% gave her chances that might win the 2010 elections, while 53% unfavour her.

Thursday, 18 November 2010
CHADEMA Wamsusa Rais Kikwete na Kuondoka Bungeni
Katika hali isiyokuwa ya kutarajiwa, Wabunge wa CHADEMA leo wameondoka ndani ya ukumbi wa Bunge mara tu Rais Jakaya Kikwete alipokuwa anataka kuanza kuhutubia bunge la 10.
Kwa muda wote wakati rais anaingia na muda wa kusoma dua, wabunge wote walikuwa wametulia. Lakini mara tu rais Kikwete alipoanza kuongea, wabunge wa CHADEMA wakaamka ghafla na kutoka nje huku kukiwa na kelele za mzomeo na wabunge wa CCM wakiwaonyesha mikono kwa kupunga wakimaanisha waondoke tu!
Bado sababu halisi ya kumsusa Rais Kikwete haijawekwa hadharani, japo ilikuwa inajulikana ya kuwa uongozi wa CHADEMA ulikuwa unadai rais Kikwete hakushinda kihalali kutokana na ubovu wa uendeshaji wa tume ya uchaguzi ya taifa, huku wakiwa wanaituhumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya uchakachuaji wa kura kutoka kwa baadhi ya maofisa wake na kuipendelea CCM huku wakiihujumu CHADEMA.
Majuzi, spika wa bunge la Tanzania, Anne Makinda, aliwaita viongozi wawili wa kambi ya upinzani kutoka CHADEMA na kuwasihi wakubali kumtambua Rais Kikwete kama kiongozi halali wa Tanzania vinginevyo wanaweza kupoteza haki zao za msingi za kuwawakilisha vyema wananchi waliowachagua. Hatima ya kikao hiki cha faragha hazikujulikana wazi.

Subscribe to:
Posts (Atom)