Thursday, 30 September 2010
Tuesday, 28 September 2010
Monday, 27 September 2010
Kenya Airways: Nao Wamo Kwa Ndege za Mitumba
Nilikuwa kimya kwa siku kadhaa, kwani nilikuwa mimekabiliwa na majukumu yanayohusu mipango ya maendeleo na utoaji huduma za macho, mpango huu unahusisha juhudi binafsi za wananchi wazalendo na wazawa katika ukanda wa Afrika Mashariki, na kwa kuanzia, Kenya ndio imekuwa ya kwanza kuratibu mpango huu kwa nchi shirikishi za umoja huu wa kanda ya Afrika Mashariki.Kwa kuwa nilikabiliwa na zaidi ya masaa 40 bila ya kulala kutokana na usafiri kuanza saa 6 usiku na kuondoka usiku wa manane ilhali mkutano ulikuwa unaanza saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku, na baada ya hapo kuandika muhtasari.. hakika siwezi kusema zaidi........
kusafiri, ni kuona mengi na pia kujifunza mengi. Hapo jana wakati narejea Kigali, nilipokuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi, niliona ndege kwa mbali, nikadhani ni ya KLM, lakini kwa kuwa nimezoea kuona madege ya KLM ambayo huja huku, nikashangaa kwa nini safari hii wameleta ndege ndogo, tena jioni.. ..... wakati huwa zinatua huku usiku na kuondoka usiku huo huo..... nikawa na maswali...
Kusoma jina la ndege likawa halifanani na rangi ya ndege niliyoizoea!, nilihisi bado nina usingizi, na hivyo rangi zikawa zinanichanganya. Nilipata moyo baada ya kuona kuna baadhi ya wasafiri wenzangu nao walikuwa wakishangaa kama mimi. Wengine walikuwa wakikenua meno na kucheka, kwani nao naona walikuwa wanshangaa hizo rangi za ndege kuwa ni za KLM wakati shirika linaloimiliki ni Kenya Airways
Tukutane tena wakati mwingine, kwani safari hii ilinifurahisha kwa mengi ambayo iliniwezesha kukaa miji mitatu, kwenye nchi tatu tofauti kwa siku moja!!
Friday, 24 September 2010
Google translator Ruins Swahili-English Meaning
Many people have been laughing when reviewing or translating swahili words into English by using google translator...
I did not pay critical attention regarding these translations until recently when I tried to translate what I had written using google translator.
What came out of it... ugh!....senseless meaning, in fact, if you know well swahili language, you may think something is wrong with your computer or your eyes :-)
It is my hope that google company will review swahili vocabularly and put more appropriate words to enable appropriate translation.

Wednesday, 22 September 2010
Vituko Bongo: Mwanaume Mmbeya "Aolewa"
Bongo... kila kukicha hakuishi vituko
Kuna habari hii iliyoandikwa kwenye Global publishers ambapo mwanaume mmoja tena ambaye ana mke, amekuwa na tabia ya kuwapigia simu wake wa wanaume ambao anawajua pindi tu anapowakuta wamesimama mahali popote na mwanamke mwingine
Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 17, 2010 Sinza ya Kumekucha jijini Dar es Salaam jirani kabisa na hoteli ya Lion ambako mwanaume aliyedaiwa kufanyiwa kitendo hicho anaishi.
Msafara wa magari ya kifahari yapatayo kumi na tano yaliwasili nyumbani kwa mwanaume huyo ndani yake kukiwa na waalikwa walioonekana kuwa na furaha za shamrashamra hizo.
Msafara huo ulipofika nje ya nyumba ya mwanaume huyo mwenye mke ulisimama huku matarumbeta yakipulizwa na watu wakiserebuka kwa ngoma ya Baikoko iliyokodishwa toka jijini Tanga.
Hata hivyo, ilidaiwa kwamba mwanaume huyo ambaye bado kijana alipochungulia nje na kuona wageni akiwemo ‘bwanaharusi’ aliingia mitini kwa kutumia mlango wa nyuma kwani toka jana yake alishanyetishiwa kuwepo kwa ‘ndoa’ hiyo ya aina yake.
Akiongea na waandishi wetu eneo la tukio, mmoja wa wageni waalikwa (hakupenda kutaja jina lake) alisema kuwa, wamealikwa katika sherehe ya ‘ndoa’ ya kijana huyo kwa lengo la kumshikisha adabu na kuachana na tabia yake ya ambea mtaani anakoishi.

Leo Katika Kona ya Siasa: Dr Faustine Ndugulile
![]() |
| Dr Faustine Ndugulile, wakati akitambulishwa na JK kwa wakazi wa Kigamboni siku ya uzinduzi rasmi wa Kampeni jimbo la Kigamboni |
Dr Faustine akimwaga sera katika harakati za kuomba kura
Safari ya kugombea ubunge si kazi ndogo.
Inahitaji maandalizi ya kutosha, uelewa wa hali ya juu kuhusu matatizo ya wananchi unaotaka kuwawakilisha, nia ya dhati katika kuyatatua matatizo bila kutanguliza maslahi yako binafsi na ahadi zinazotekelezeka.
Kwani kipimo cha imani ya wananchi unaotaka kuwawakilisha, kitaoanisha ahadi zako na utekelezaji wake.
Safari hii ya kupata ridhaa ya wananchi pia inazua maadui kwa sababu mbalimbali zikiwamo tofauti za kisera na pia maslahi binafsi.
Inahitaji moyo wa dhati, dhamira ya kweli na utashi wa kimawazo kutimiza matumaini ya watu. Na pia inahitaji uimara na msimamo thabiti katika ukweli unaouamini.
Chagua mtu atakaye kufaa na kukuwakilisha vyema.
Habari hii Imenukuliwa kutoka kwa mwanasiasa
Tuesday, 21 September 2010
Posting Comments
Dear my readers.
I will do very little modification on posting comments to this blog.
This is because of overwhelming spams especially on my older posts.
If this will not solve the problem, later on, I will be forced to put comments moderation which I understand will delay your comments to be posted especially at the time where I will not be able to access my mails.
Tupo pamoja

Sunday, 19 September 2010
Watoto walemavu wa Tanzania Watumika Kama Kitega Uchumi Kenya
Juzi jioni mtanzania mmoja ambaye anaishi jijini Nairobi kwa muda mrefu sasa aliyejulikana kwa jina la Yohana Kulwa pamoja na mkewe raia wa Kenya walikamatwa na makachero wa Kenya baada ya kugundulika kuwa alikuwa anawatumia watoto walemavu kutoka Tanzania kama mradi wa kujipatia kipato.
Watoto hao wadogo chini ya miaka 10, wamekuwa wakichukuliwa na gari kutoka nyumbani kwa Yohana saa 10 alfajiri mpaka katikati ya Jiji la Nairobi, na kisha wanapakiwa kwenye mkokoteni ambao huanza kuwasambaza sehemu mbalimbali za Jiji la Nairobi ambazo zinapitwa na watu wengi.
Watoto hao hukaa wakiomba kuanzia asubuhi mpaka jioni bila hata chakula, ikifika muda wa saa 9 alasiri, wengi huwa wamechoka sana na njaa, na hivyo kupitiwa na usingizi, ukizingatia huamshwa mapema karibu ya saa 9 usiku.
Ifikapo jioni, watoto hao hujisogeza taratibu kwa kujivuta barabarani hadi kwenye sehemu ambapo gari hilo huja kuwachukua.
Watu walio kwenye mtandao huo, huwa wajanja, kwani jioni uhakikisha ya kuwa mwendesha mkokoteni yupo karibu, ambapo hutumika kukinga watu wasione hao watoto wanapopakiwa kwenye gari na kurudishwa kwa tapeli huyo wa Kitanzania na mkewe.
Siku polisi walipowafuatilia walimkuta mtanzania huyo na mkewe wakiwa wanagalia runinga kwa starehe zao, huku walemavu wao wakiingizwa ndani mmoja mmoja.
Polisi walipohesabu pesa walizoingia nazo hao siku hiyo, walipata jumla ya KSh zaidi ya 13,000 (Karibu ya dola za marekani 150), na inasemekana kila siku watoto hao huja na kiasi kama hicho.
Uchunguzi wa polisi bado unaendelea, na inatarajiwa wezi hawa watafikishwa mahalamani wiki ijayo.
Wakati huo huo, polisi wa Kenya, jana wamekamata watu wengine tena ambao hutumia chokoraa pia kwa mtindo huo huo kwa kuwatumia kama nguvu kazi, tofauti ni kuwa watoto hawa sio walemavu, na walikutwa na jumla ya zaidi ya ksh 2,000 kama makusanyo ya siku hiyo ya jana.
Kwa mtazamo wangu:
Huyo mtanzania anatakiwa kupata adhabu kali, si ajabu aliwachukua watoto hao toka kwa wazazi wao kwa kuwadanganya ya kuwa anawapeleka kusoma au ....., kumbe ni tapeli mkubwa
NB. Watoto hao walionyeshwa kwenye runinga ya Citizen tangu wanachukuliwa na gari dogo asubuhi, kubebwa kwenye mkokoteni, wakiwa kazini, jioni walipokuja kuchukuliwa na mwisho wakati Mtanzania huyo alipokamatwa na mkewe. Na matapeli hao walikiri kufanya mchezo mchafu huo.

Subscribe to:
Posts (Atom)