Monday, 13 December 2010

Gwiji la Muziki Remmy Mtoro Ongala Afariki Dunia

Mwananmziki mkongwe na maarufu nchini Tanzania, Ramadhani Mtoro Ongala au maarufu kama Dokta Remmy amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.  
  
Remmy alikuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kisukari ambao ulisababishwa alazwe mara kadhaa hospitalini ikiwa ni pamoja na hospitali ya taifa ya Muhimbili. Inasemekana amefariki kwa matatizo hayo hayo ya kisukari.  
   
Remmy atakumbukwa kwa mengi ikiwa ni pamoja na kuwa mshindi wa pili kwa sura mbaya Tanzania japo alilalamika ya kuwa kaonewa kwani aliamini ya kuwa yeye ana sura mbaya kuliko watu wote waliokuwa wanaishi Tanzania wakati huo!!!!!  
  
Pia kuna nyimbo kadhaa alizoimba ambazo watu watatzikumbuka ikiwa ni pamoja na wimbo wa KIFO. 
 
Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi

5 comments:

  1. Astarehe kwa amani ametangulia nasi tutakuja huko huko. Amina

    ReplyDelete
  2. Amina, katangulia mbele za haki!

    ReplyDelete
  3. RIP dokta remmy.

    kati ya nyimbo zake huwa sichoki kuusikiliza 'Karola'

    kipande cha kwanza kinaenda hivi:

    "Ukiwa mtenda mabaya
    wewe mwenyewe haujijui
    Ukiwa mtenda mabaya
    kila siku unasema unaonewa
    Ukiwa mtenda mabaya
    huko unakokwenda ni pabaya
    Ukiwa na roho mbaya eeh
    kweli tutakuogopa
    Ukiwa na pesa nyingi
    usahau hata ndugu zako
    kweli walimwengu hawana wema
    Mola awape nini"

    katika wimbo huu tumba, saxaphone na solo guitar la yeye mwenyewe huwa vinanikuna. hasa tumba.

    Remmy Ongala katutangulia lakini nyuma kaacha kielelezo cha muziki wa dansi iliyo hai. Kifo chake kinathibitisha kutokomea muziki wa dansi na kushamiri huu wa "ubongo wa fleva"

    hakika ni pengo

    Hilo la sura mbaya liliteta zogo nchini tanzania. mshindi aliitwa masoud. dk remmy alidai kuwa masoud hakuwa na sura mbaya bali alikuwa na maradhi ya ngozi ya usoni. kama sijasahau wa tatu alikuwa mzee jangala.

    ReplyDelete