Saturday, 5 December 2009

Hongera Mama


Lao mama wa kibaraza hiki anasheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Niseme nini tena..... Kama si yeye, wewe msomaji usingepata fursa ya kukodolea macho Hadubini.
Ninamtakia afya njema, na mwakani tena tusheherekee sikukuu kama hii.
God bless

13 comments:

  1. Hongera sana mama Mungu akuzidishie afya njema

    ReplyDelete
  2. namtakia maisha marefu na afya njema.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana mama,
    Wewe ni kitu chema,
    Kumleta Chib mwema,
    Ahsante twakupatia.

    Chib rafiki yetu,
    Tena kajaa utu,
    Mpiganaji miongoni mwetu,
    Ambaye twajivunia.

    Mama tukulipe nini?
    Kufikia yako thamani,
    Hakuna kitu duniani,
    Thamani kukufikia.

    Mungu na akujalie,
    Maisha uyafurahie,
    Miaki mingi ufikie,
    Katika hii dunia.

    ReplyDelete
  4. Hongera kwa Mama mzaa chema!

    ReplyDelete
  5. Natumaini Mama kaongeza siku kwa salamu zote hizi.
    Nawashukuru wote kwa kuungana nasi.
    Kaka Fadhy, shukrani kwa shairi lako. Itabidi mama aanze ku-blog ili naye apate vionjo vya blog. :-)

    ReplyDelete
  6. habari hazizeeki kwa anayeipata sasa na mimi kwa falsafa hiyohiyo salamu zangu za pongezi hazijazeeka ingawaje nimetoa kwa kuchelewa. chelewa ufike. hongera mama.

    swali: hivi 'hadubini my-o-scope' maana yake nini?

    ReplyDelete
  7. Dukuduku langu lipo hapo hapo alipogusia Mwaipopo!

    ReplyDelete
  8. Hata na mimi ndio dukuduku langu lipo hapo alipogusia Mwaipopo!!

    ReplyDelete
  9. Hongera Mama !

    - ingawa nimechelewa kutoa hongera HASA kwa kujihami kuwa nimechelewa kutoa hongera.!

    ReplyDelete